top of page

      July 15 LITURGY
         host: Kenya
presider: Fr Mahoussi

ENTRANCE
Twimbe Kwa Shangwe Lyrics

 

Twimbe kwa shangwe na furaha *2

Bwana ametufanyia makuu

 

Tuingie kwake Mungu wetu,

Tuingie kwake kwa shukrani,

Bwana ametufanyia makuu

 

Yeye ndiye Mungu wa miungu,

Yeye ndiye Bwana wa mabwana,

Bwana ametufanyia makuu

 

Bwana ni mfalme wa wafalme,

Yeye ndiye Baba wa viumbe,

Bwana ametufanyia makuu

 

Ametenda mambo ya ajabu,

Aliye gizani hatajua,

Bwana ametufanyia makuu

 

Tuingie kwake Muumba wetu

Tuingie kwake kwa shukrani

Bwana ametufanyia makuu

 

Sifa na heshima kwake Mungu

Mwenye utukufu wa ajabu

Bwana ametufanyia makuu

 

2.UTUHURUMIE (MISA KARIOBANGI)

 [ v ] Utuhurumie

[ w ] Ee Bwana, ee Bwana, ee Bwana

[ v ] Tuhurumie

[ w ] Ee Bwana, ee Bwana, ee Bwana, Bwana utuhurumie

 

Utuhurumie

Ee Kristu, ee Kristu, ee Kristu

Tuhurumie

Ee Kristu, ee Kristu, ee Kristu, Kristu utuhurumie

 

 

3. BIBLE PROCESSION (Kenyan Style)

Inasonga Mbele Lyrics

 

Inasonga mbele injili yetu ulimwenguni kote -

Neno laenda mbele *2

 

Injili - (iende mbele Injili yake Yesu *2) *2

{Inasonga mbele - Injili *2 yake Yesu *2}

 

Inasonga mbele injili yetu katika mataifa -

Inasonga mbele injili yetu katika makabila -

 

Inasonga mbele Injili yetu katika jumuiya

GOSPEL

 

HOMILY:  Margaret Gonsalves

 

4. Sadaka

Beba Mikononi Lyrics

 

Tusimame ndugu twende kwake Bwana (kweli)

Usisite ndugu amka twende hima

 

Beba mikononi (mwako) uliyojaliwa

Peleka kwa Bwana, upate Baraka

 

Peleka kwa moyo, moyo wa mapendo (kweli)

Peleka kwa Bwana uliyojaliwa

 

Sadaka ya fedha, fedha za mifuko (ndugu)

Amka upeleke mezani kwa Bwana

 

Mavuno mifugo, ni mali ya Bwana (kweli)

Tupeleke kwake atazipokea

 

Mkate divai tupeleke kwake (leo)

Tupate baraka mbele zake Bwana

 

Twende ndugu twende, mbele zake Bwana (twende)

Tupeleke nafsi zetu kwake Bwana

5.Mtakatifu (miss Kariobangi)

[b] Mtakatifu

[w]: Mtakatifu Mtakatifu Bwana Mungu

[b] Wa majeshi

[w] Mbingu na dunia zimejaa tukufu wak

Hosanna, Hosanna juu Mbinguni

[Hosanna] Hosanna juu Mbinguni

Mbarikiwa

Anayekuja kwa jina lake Bwana Mungu

6. FUMBO LA IMANI (MISA KARIOBANGI)

 

Kristu - alikufa, Kristu - alifufuka

Kristu Yesu - alikufa, alifufuka, atakuja tena

 

7.BABA YETU (MISA KARIOBANGI)

 

Baba yetu uliye Mbinguni, Jina lako litukuzwe

Ufalme wako ufike utakalo lifanyike

 

Duniani kama Mbinguni -utakalo lifanyike

Tupe leo mkate wetu -

Mkate wetu wa kila siku -

 

Tusamehe makosa yetu -

Kama vile twawasamehe -

Waliotukosea sisi -

Situtie majaribuni -

Walakini utuopoe -

Maovuni utuopoe -

Kwa kuwa ufalme ni wako -

Na nguvu na utukufu -

Utukufu hata milele -

 

8.EE MWANA KONDOO (MISA KARIOBANGI)

 

[ S ] Ee Mwana kondoo

[ w ] Uondoaye dhambi za dunia utuhurumie } *2

 

Ee Mwanakondo . . .y

 

Ee Mwana kondoo

Uondoaye dhambi za dunia utujalie amani

 

9. COMMUNION

 

10.THANKSGIVING

Natamani Kuruka Lyrics

 

(Nipishe Njia)

 

Nipishe njia nipeni nafasi

Nimuonyeshe Mungu nilivyofurahi

Nitamwimbia ngoma nitacheza

Nimuonyeshe Mungu nilivyofurahi

 

Natamani kuruka, nifika kule

Nimuinue Mungu kwa mikono yangu

Nimueleze kwa kinywa, changu mwenyewe

Kwamba nimefurahi kwa upendo wake

Bwana nashukuru, nashukuru nashukuru tu

Ninashukuru kwa kunipenda bila mwisho

Sina cha kusema, cha kusema cha kusema tu

Ninashukuru kwa kunipenda bila mwisho

 

Kaniinua kutoka shimoni -

Akaniweka juu ya kinara -

Nitazunguka kwa maringo tele -

Na tabasamu lisilo kauka -

 

Nitawashika wenzangu mikono -

Tujiinue juu kwa pamoja -

Wenzangu si mmejionea wenyewe -

Mungu alivyo mwema wa ajabu -

 

Nitaandika utukufu wake -

Na wajukuu wangu wausome -

 

11.EXIT

Jina Maria Lyrics

Jina Maria jina tukufu lafurahisha latuliza

Hata malaika wanaliimba,

Ave ave Maria, Ave ave ave Maria

Wakisema (siku zote) bila mwisho

Ave Maria! Ave ave ave Maria

 

Jina Maria jina tukufu, lafurahisha la tutuliza

Jina Maria jina tukufu, latuletea neema ya Mungu

Jina Maria jina tukufu, lawafukuza pepo wabaya

 

Jina Maria jina tukufu, lawapendeza watakatifu 

bottom of page